Read Kolonia Santita by Enock Maregesi Free Online


Ebook Kolonia Santita by Enock Maregesi read! Book Title: Kolonia Santita
The size of the: 37.56 MB
Edition: Authorhouse
Date of issue: September 13th 2012
ISBN: 1477222960
ISBN 13: 9781477222966
The author of the book: Enock Maregesi
Language: English
Format files: PDF

Read full description of the books:

'Kolonia Santita: Laana Ya Panthera Tigrisi' ni hadithi ya kusisimua ya kijasusi na madawa ya kulevya iliyoandikwa na Enock Abiud Maregesi. Inazungumzia vita kati ya Tume ya Dunia ya Umoja wa Mataifa, ya kudhibiti madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa, 'World Drugs Enforcement Commission' (WODEC) au Tume ya Dunia; na shirika kubwa la madawa ya kulevya la Kolonia Santita (CS-14) la Kolombia na Meksiko. Inaelezea, kwa kinagaubaga, jitihada za pamoja kati ya Tume ya Dunia, Marekani na Meksiko za kuwasaka na hatimaye kuwatia nguvuni viongozi nduli wa CS-14; na kuzuia shehena (kubwa) ya madawa ya kulevya na malighafi ya nyukilia: kwenda Afrika, Asia, Amerika, Ulaya – na kung’oa mizizi ya shirika la CS-14, lote, katika nchi za Hemisifi a ya Magharibi – na duniani kwa jumla.
Hiki ni kitabu cha kwanza cha aina yake cha kimataifa katika Tanzania. Lengo lake si tu kukata kiu ya wapenzi wa riwaya za kipelelezi na kufufua mwamko wa usomaji wa vitabu; ni kuleta, hali kadhalika, ufahamu na burudani ya kimataifa kwa Watanzania, Wakenya na Waganda – na jamii nzima ya Afrika ya Mashariki inayozungumza Kiswahili – na walowezi wa jamii yote ya Kiswahili duniani.

Read Ebooks by Enock MaregesiRead information about the author

Ebook Kolonia Santita read Online! Enock Maregesi was born in Tanzania. He is the author of KOLONIA SANTITA, a novel. In 2015 he won the Mabati-Cornell Kiswahili Prize For African Literature for KOLONIA SANTITA. The prize has the express goal in recognizing excellent writing in African languages and encourages translation from, between and into African languages! He lives in Tanzania.

Enock Maregesi alizaliwa nchini Tanzania. Amesomea teknolojia ya habari na utawala wa biashara katika Chuo Kikuu cha Wales, na uandishi wa habari na vitabu katika chuo cha ubunifu wa kifasihi cha Manchester (The Writers Bureau) nchini Uingereza. Hadithi ya KOLONIA SANTITA: LAANA YA PANTHERA TIGRISI ni kitabu chake cha kwanza kilichohamasishwa na wakongwe wa riwaya wa Tanzania - kama Elvis Musiba, Euphrase Kezilahabi na Ben Mtobwa - na utafiti yakinifu wa miaka kumi na nane wa ujasusi, madawa ya kulevya, ugaidi wa kimataifa na silaha za maangamizi za kikemia na kibiolojia. Alizaliwa huko Mwanza mwaka 1972 na kukulia Musoma na Dar es Salaam ambako anaishi mpaka leo, akijishughulisha na biashara na uandishi wa vitabu.Ebooks PDF EpubAdd a comment
Read EBOOK Kolonia Santita by Enock Maregesi Online free

Download PDF: kolonia-santita.pdf Kolonia Santita PDF